1. |
Itakapo tetemeshwa ardhi kwa mtetemeko wake! |
2. |
Na itakapo toa ardhi mizigo yake! |
3. |
Na mtu akasema: Ina nini? |
4. |
Siku hiyo itahadithia khabari zake. |
5. |
Kwa sababu Mola wake Mlezi ameifunulia! |
6. |
Siku hiyo watu watatoka kwa mfarakano wakaonyweshwe vitendo vyao! |
7. |
Basi anaye tenda chembe ya wema, atauona! |
8. |
Na anaye tenda chembe ya uovu atauona! |