1. |
Hakika Sisi tumeiteremsha Qur’ani katika Laylatul Qadri, Usiku wa Cheo Kitukufu. |
2. |
Na nini kitacho kujuulisha nini Laylatul Qadri? |
3. |
Laylatul Qadri ni bora kuliko miezi elfu. |
4. |
Huteremka Malaika na Roho katika usiku huo kwa idhini ya Mola wao Mlezi kwa kila jambo. |
5. |
Amani usiku huo mpaka mapambazuko ya alfajiri. |