1. |
Naapa kwa mchana! |
2. |
Na kwa usiku unapo tanda! |
3. |
Mola wako Mlezi hakukuacha, wala hakukasirika nawe. |
4. |
Na bila ya shaka wakati ujao utakuwa bora kwako kuliko ulio tangulia. |
5. |
Na Mola wako Mlezi atakupa mpaka uridhike. |
6. |
Kwani hakukukuta yatima akakupa makaazi? |
7. |
Na akakukuta umepotea akakuongoa? |
8. |
Akakukuta mhitaji akakutosheleza? |
9. |
Basi yatima usimwonee! |
10. |
Na anaye omba au kuuliza usimkaripie! |
11. |
Na neema za Mola wako Mlezi zisimlie. |