1. |
Naapa kwa usiku unapo funika! |
2. |
Na mchana unapo dhihiri! |
3. |
Na kwa Aliye umba dume na jike! |
4. |
Hakika juhudi zenu bila ya shaka ni mbali mbali. |
5. |
Ama mwenye kutoa na akamchamngu, |
6. |
Na akaliwafiki lilio jema, |
7. |
Tutamsahilishia yawe mepesi. |
8. |
Na ama mwenye kufanya ubakhili, na asiwe na haja ya wenzake, |
9. |
Na akakanusha lilio jema, |
10. |
Tutamsahilishia yawe mazito! |
11. |
Na mali yake yatamfaa nini atapo kuwa anadidimia? |
12. |
Hakika ni juu yetu kuonyesha uwongofu. |
13. |
Na hakika ni yetu Sisi Akhera na dunia. |
14. |
Basi nakuonyeni na Moto unao waka! |
15. |
Hatauingia ila mwovu kabisa! |
16. |
Anaye kadhibisha na kupa mgongo. |
17. |
Na mchamngu ataepushwa nao, |
18. |
Ambaye hutoa mali yake kwa ajili ya kujitakasa. |
19. |
Na wala si kwa kuwa yupo yeyote aliye mfanyia hisani ndio anamlipa. |
20. |
Ila ni kutaka radhi ya Mola wake Mlezi aliye juu kabisa. |
21. |
Naye atakuja ridhika! |