1. |
Naapa kwa Mji huu! |
2. |
Nawe unaukaa Mji huu. |
3. |
Na naapa kwa mzazi na alicho kizaa. |
4. |
Hakika tumemuumba mtu katika taabu. |
5. |
Ati anadhani hapana yeyote ataye muweza? |
6. |
Anasema: Nimeteketeza chungu ya mali. |
7. |
Ati anadhani ya kuwa hapana yeyote anaye mwona? |
8. |
Kwani hatukumpa macho mawili? |
9. |
Na ulimi, na midomo miwili? |
10. |
Na tukambainishia zote njia mbili? |
11. |
Lakini hakujitoma kwenye njia ya vikwazo vya milimani. |
12. |
Na nini kitakujuvya ni nini njia ya vikwazo vya milimani? |
13. |
Kumkomboa mtumwa; |
14. |
Au kumlisha siku ya njaa |
15. |
Yatima aliye jamaa, |
16. |
Au masikini aliye vumbini. |
17. |
Tena awe miongoni mwa walio amini na wakausiana kusubiri na wakausiana kuhurumiana. |
18. |
Hao ndio watu wa kheri wa kuliani. |
19. |
Lakini walio zikataa Ishara zetu, hao ndio watu wa shari wa kushotoni. |
20. |
Juu yao utakuwa Moto ulio fungiwa kila upande. |