1. |
Litakase jina la Mola wako Mlezi aliye juu kabisa, |
2. |
Aliye umba, na akaweka sawa, |
3. |
Na ambaye amekadiria na akaongoa, |
4. |
Na aliye otesha malisho, |
5. |
Kisha akayafanya makavu, meusi. |
6. |
Tutakusomesha wala hutasahau, |
7. |
Ila akipenda Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye anayajua yaliyo dhaahiri na yaliyo fichikana. |
8. |
Na tutakusahilishia yawe mepesi. |
9. |
Basi kumbusha, kama kukumbusha kunafaa. |
10. |
Atakumbuka mwenye kuogopa. |
11. |
Na atajitenga mbali nayo mpotovu, |
12. |
Ambaye atauingia Moto mkubwa. |
13. |
Tena humo hatakufa wala hawi hai. |
14. |
Hakika amekwisha fanikiwa aliye jitakasa. |
15. |
Na akakumbuka jina la Mola wake Mlezi, na akasali. |
16. |
Lakini nyinyi mnakhiari maisha ya dunia! |
17. |
Na Akhera ni bora na yenye kudumu zaidi. |
18. |
Hakika haya yamo katika Vitabu vya mwanzo, |
19. |
Vitabu vya Ibrahimu na Musa. |