1. |
Naapa kwa mbingu na Kinacho kuja usiku! |
2. |
Na nini kitakacho kujuulisha ni nini hicho Kinacho kuja usiku? |
3. |
Ni Nyota yenye mwanga mkali. |
4. |
Hapana nafsi ila inayo mwangalizi. |
5. |
Hebu naajitazame mwanaadamu ameumbwa kwa kitu gani? |
6. |
Ameumbwa kwa maji yatokayo kwa kuchupa, |
7. |
Yatokayo baina ya mifupa ya mgongo na mbavu. |
8. |
Hakika Yeye ana uweza wa kumrudisha. |
9. |
Siku zitakapo dhihirishwa siri. |
10. |
Basi hatakuwa na nguvu wala msaidizi. |
11. |
Naapa kwa mbingu yenye marejeo! |
12. |
Na kwa ardhi inayo pasuka! |
13. |
Hakika hii ni kauli ya kupambanua. |
14. |
Wala si mzaha. |
15. |
Hakika wao wanapanga mpango. |
16. |
Na Mimi napanga mpango. |
17. |
Basi wape muhula makafiri – wape muhula pole pole. |