1. |
Itapo chanika mbingu, |
2. |
Na ikamsikiliza Mola wake Mlezi, na ikapasiwa kumsikiliza, |
3. |
Na ardhi itakapo tanuliwa, |
4. |
Na kuvitoa vilivyo kuwa ndani yake, ikawa tupu, |
5. |
Na ikamsikiliza Mola wake Mlezi, na ikapasiwa kumsikiliza, |
6. |
Ewe mtu! Hakika wewe unajikusuru kwa juhudi kumwendea Mola wako Mlezi, basi utamkuta. |
7. |
Ama atakaye pewa daftari lake kwa mkono wa kulia, |
8. |
Basi huyo atahisabiwa hisabu nyepesi, |
9. |
Na arudi kwa ahali zake na furaha. |
10. |
Na ama atakaye pewa daftari lake kwa nyuma ya mgongo wake, |
11. |
Basi huyo ataomba kuteketea. |
12. |
Na ataingia Motoni. |
13. |
Hakika alikuwa furahani kati ya jamaa zake. |
14. |
Huyo hakika alidhani kuwa hatarejea tena. |
15. |
Kwani? Hakika Mola wake Mlezi alikuwa akimwona! |
16. |
Basi ninaapa kwa wekundu wa jua linapo kuchwa, |
17. |
Na kwa usiku na unavyo vikusanya, |
18. |
Na kwa mwezi unapo pevuka, |
19. |
Lazima mtapanda t’abaka kwa t’abaka! |
20. |
Basi wana nini hawaamini? |
21. |
Na wanapo somewa Qur’ani hawasujudu? |
22. |
Bali walio kufuru wanakanusha tu. |
23. |
Na Mwenyezi Mungu anajua wanayo yadhamiria. |
24. |
Basi wabashirie adhabu chungu! |
25. |
Isipo kuwa wale walio amini na wakatenda mema; hao watakuwa na ujira usio malizika. |