1. |
Mbingu itapo chanika, |
2. |
Na nyota zitapo tawanyika, |
3. |
Na bahari zitakapo pasuliwa, |
4. |
Na makaburi yatapo fukuliwa, |
5. |
Hapo kila nafsi itajua ilicho tanguliza, na ilicho bakisha nyuma. |
6. |
Ewe mwanaadamu! Nini kilicho kughuri ukamwacha Mola wako Mlezi Mtukufu? |
7. |
Aliye kuumba, akakuweka sawa, akakunyoosha, |
8. |
Katika sura yoyote aliyo ipenda akakujenga. |
9. |
Sivyo hivyo! Bali nyinyi mnaikanusha Siku ya Malipo. |
10. |
Na hakika bila ya shaka wapo walinzi juu yenu, |
11. |
Waandishi wenye hishima, |
12. |
Wanayajua mnayo yatenda. |
13. |
Hakika wema bila ya shaka watakuwa katika neema, |
14. |
Na hakika waovu bila ya shaka watakuwa Motoni; |
15. |
Wataingia humo Siku ya Malipo. |
16. |
Na hawatoacha kuwamo humo. |
17. |
Na nini kitakacho kujuulisha Siku ya Malipo ni siku gani? |
18. |
Tena nini kitakacho kujuulisha Siku ya Malipo ni siku gani? |
19. |
Siku ambayo nafsi haitakuwa na madaraka yoyote juu ya nafsi; na amri yote siku hiyo ni ya Mwenyezi Mungu tu. |