1. |
Jua litakapo kunjwa, s |
2. |
Na nyota zikazimwa, |
3. |
Na milima ikaondolewa, |
4. |
Na ngamia wenye mimba pevu watakapo achwa wasishughulikiwe, |
5. |
Na wanyama wa mwituni wakakusanywa, |
6. |
Na bahari zikawaka moto, |
7. |
Na nafsi zikaunganishwa, |
8. |
Na msichana aliye zikwa hai atapo ulizwa, |
9. |
Kwa kosa gani aliuliwa? |
10. |
Na madaftari yatakapo enezwa, |
11. |
Na mbingu itapo tanduliwa, |
12. |
Na Jahannamu itapo chochewa, |
13. |
Na Pepo ikasogezwa, |
14. |
Kila nafsi itajua ilicho kihudhurisha. |
15. |
Naapa kwa nyota zinapo rejea nyuma, |
16. |
Zinazo kwenda, kisha zikajificha, |
17. |
Na kwa usiku unapo pungua, |
18. |
Na kwa asubuhi inapo pambazuka, |
19. |
Kwamba hakika bila ya shaka hii ni kauli ya Mjumbe mtukufu, |
20. |
Mwenye nguvu na mwenye cheo kwa huyo Mwenye Kiti cha Enzi, |
21. |
Anaye t’iiwa, tena muaminifu. |
22. |
Na wala huyu mwenzenu hana wazimu. |
23. |
Na hakika yeye alimwona kwenye upeo wa macho ulio safi. |
24. |
Wala yeye si bakhili kwa mambo ya ghaibu. |
25. |
Wala hii si kauli ya Shetani maluuni. |
26. |
Basi mnakwenda wapi? |
27. |
Haikuwa hii ila ni ukumbusho kwa walimwengu wote. |
28. |
Kwa yule miongoni mwenu anaye taka kwenda sawa. |
29. |
Wala nyinyi hamtataka isipo kuwa atake Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu wote. |