1. |
Naapa kwa zinazo tumwa kwa upole! |
2. |
Na zinazo vuma kwa kasi! |
3. |
Na zikaeneza maeneo yote! |
4. |
Na zinazo farikisha zikatawanya! |
5. |
Na zinazo peleka mawaidha! |
6. |
Kwa kuudhuru au kuonya, |
7. |
Hakika mnayo ahidiwa bila ya shaka yatakuwa! |
8. |
Wakati nyota zitakapo futwa, |
9. |
Na mbingu zitakapo pasuliwa, |
10. |
Na milima itakapo peperushwa, |
11. |
Na Mitume watakapo wekewa wakati wao, |
12. |
Kwa siku gani hiyo wamewekewa muda huo? |
13. |
Kwa siku ya kupambanua! |
14. |
Na nini kitakacho kujuulisha siku ya kupambanua ni nini? |
15. |
Ole wao, siku hiyo hao wanao kanusha! |
16. |
Kwani hatukuwaangamiza walio tangulia? |
17. |
Kisha tukawafuatilizia walio fuatia? |
18. |
Ndio kama hivi tuwatendavyo wakosefu! |
19. |
Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha! |
20. |
Kwani hatukukuumbeni kwa maji ya kudharauliwa? |
21. |
Kisha tukayaweka mahali pa utulivu madhubuti? |
22. |
Mpaka muda maalumu? |
23. |
Tukakadiria na Sisi ni wabora wa kukadiria. |
24. |
Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha! |
25. |
Kwani hatukuifanya ardhi yenye kukusanya |
26. |
Walio hai na maiti? |
27. |
Na ndani yake tukaweka milima mirefu yenye kuthibiti, na tunakunywesheni maji matamu? |
28. |
Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha! |
29. |
Nendeni kwenye adhabu mliyo kuwa mkiikanusha! |
30. |
Nendeni kwenye kivuli chenye mapande matatu! |
31. |
Hakikingi moto, wala hakiwaepushi na mwako. |
32. |
Hakika Moto huo unatoa macheche kama majumba! |
33. |
Kama kwamba ni ngamia wa rangi ya manjano! |
34. |
Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha! |
35. |
Hii ni siku ambayo hawatatamka kitu, |
36. |
Wala hawataruhusiwa kutoa udhuru. |
37. |
Ole wao siku hiyo hao walio kanusha! |
38. |
Hii ndiyo siku ya kupambanua. Tumekukusanyeni nyinyi na walio tangulia. |
39. |
Ikiwa mnayo hila, nifanyieni hila Mimi! |
40. |
Ole wao siku hiyo hao walio kanusha! |
41. |
Hakika wachamngu watakuwa katika vivuli na chemchem, |
42. |
Na matunda wanayo yapenda, |
43. |
Kuleni na kunyweni kwa furaha kwa yale mliyo kuwa mkiyatenda. |
44. |
Hakika ndio kama hivyo tunavyo walipa watendao mema. |
45. |
Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha! |
46. |
Kuleni na mjifurahishe kidogo tu. Hakika nyinyi ni wakosefu! |
47. |
Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha! |
48. |
Na wakiambiwa: Inameni! Hawainami. |
49. |
Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha! |
50. |
Basi maneno gani baada ya haya watayaamini? |