1. |
Arrah’man, Mwingi wa Rehema |
2. |
Amefundisha Qur’ani. |
3. |
Amemuumba mwanaadamu, |
4. |
Akamfundisha kubaini. |
5. |
Jua na mwezi huenda kwa hisabu. |
6. |
Na mimea yenye kutambaa, na miti, inanyenyekea. |
7. |
Na mbingu ameziinua, na ameweka mizani, |
8. |
Ili msidhulumu katika mizani. |
9. |
Na wekeni mizani kwa haki, wala msipunje katika mizani. |
10. |
Na ardhi ameiweka kwa ajili ya viumbe. |
11. |
Humo yamo matunda na mitende yenye mafumba. |
12. |
Na nafaka zenye makapi, na rehani. |
13. |
Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha |
14. |
Amemuumba mtu kwa udongo wa kinamo.. |
15. |
Na akawaumba majini kwa ulimi wa moto. |
16. |
Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha |
17. |
Mola Mlezi wa mashariki mbili na wa magharibi mbili. |
18. |
Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
19. |
Anaziendesha bahari mbili zikutane; |
20. |
Baina yao kipo kizuizi, zisiingiliane. |
21. |
Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
22. |
Katika hizo bahari mbili zinatoka lulu na marijani. |
23. |
Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
24. |
Na ni vyake Yeye hivi viendavyo baharini vilivyo undwa kama vilima. |
25. |
Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
26. |
Kila kilioko juu yake kitatoweka. |
27. |
Na atabakia Mwenyewe Mola wako Mlezi Mwenye utukufu na ukarimu. |
28. |
Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
29. |
Vinamwomba Yeye vilivyomo katika mbingu na ardhi. Kila siku Yeye yumo katika mambo. |
30. |
Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
31. |
Tutakuhisabuni enyi makundi mawili. |
32. |
Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
33. |
Enyi makundi ya majini na watu! Mkiweza kupenya kwenye mbingu na ardhi, basi penyeni! Hamtapenya ila kwa kupewa madaraka. |
34. |
Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
35. |
Mtapelekewa muwako wa moto na shaba; wala hamtashinda. |
36. |
Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
37. |
Itakapo pasuka mbingu ikawa nyekundu kama mafuta. |
38. |
Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
39. |
Siku hiyo hataulizwa dhambi zake mtu wala jini. |
40. |
Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
41. |
Watajuulikana wakosefu kwa alama zao, basi watashikwa kwa nywele zao za utosini na kwa miguu. |
42. |
Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
43. |
Hii ndiyo Jahannamu ambayo wakosefu wakiikanusha. |
44. |
Watakuwa wakizunguka baina ya hiyo na maji ya moto yanayo chemka. |
45. |
Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
46. |
Na mwenye kuogopa kusimamishwa mbele ya Mola wake Mlezi atapata Bustani mbili. |
47. |
Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
48. |
Bustani zenye matawi yaliyo tanda. |
49. |
Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
50. |
Ndani yake zimo chemchem mbili zinazo pita. |
51. |
Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
52. |
Humo katika kila matunda zimo namna mbili. |
53. |
Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
54. |
Wawe wameegemea matandiko yenye bit’ana ya hariri nzito; na matunda ya Bustani hizo yapo karibu. |
55. |
Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
56. |
Humo watakuwamo wanawake watulizao macho yao; hajawagusa mtu kabla yao wala jini. |
57. |
Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
58. |
Kama kwamba wao ni yakuti na marijani. |
59. |
Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha. |
60. |
Ati yaweza kuwa malipo ya ihsani ila ihsani? |
61. |
Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
62. |
Na zaidi ya hizo zipo Bustani nyengine mbili. |
63. |
Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
64. |
Za kijani kibivu. |
65. |
Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
66. |
Na chemchem mbili zinazo furika. |
67. |
Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
68. |
Imo humo miti ya matunda, na mitende na mikomamanga. |
69. |
Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
70. |
Humo wamo wanawake wema wazuri. |
71. |
Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
72. |
Wanawake wazuri wanao tawishwa katika makhema. |
73. |
Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
74. |
Hajawagusa mtu wala jini kabla yao. |
75. |
Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
76. |
Wameegemea juu ya matakia ya kijani na mazulia mazuri. |
77. |
Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
78. |
Limetukuka jina la Mola wako Mlezi Mwenye utukufu na ukarimu. |