1. |
H’a Mim |
2. |
Naapa kwa Kitabu kinacho bainisha. |
3. |
Hakika Sisi tumeifanya Qur’ani kwa Kiarabu ili mfahamu. |
4. |
Na hakika hiyo imo katika Asili ya Maandiko yalioko kwetu, ni tukufu na yenye hikima. |
5. |
Je! Tuache kukukumbusheni kabisa kwa kuwa nyinyi ni watu mlio pita mipaka kwa ukafiri? |
6. |
Na Manabii wangapi tuliwatuma kwa watu wa zamani! |
7. |
Na hawajii Nabii yeyote ila walikuwa wakimkejeli. |
8. |
Na tuliwaangamiza walio kuwa na nguvu kushinda wao. Na mfano wa watu wa zamani umekwisha pita. |
9. |
Na ukiwauliza: Nani aliye ziumba mbingu na ardhi? Bila ya shaka watasema: Kaziumba Mwenye nguvu, Mjuzi, |
10. |
Ambaye amekufanyieni ardhi kama tandiko, na akakufanyieni ndani yake njia mpate kuongoka. |
11. |
Na ambaye ndiye aliye teremsha kutoka mbinguni maji kwa kiasi, na kwa hayo tukaifufua nchi iliyo kufa. Na namna hivi ndivyo mtakavyo tolewa. |
12. |
Na ambaye ndiye aliye umba katika kila kitu jike na dume, na akakufanyieni marikebu na wanyama mnao wapanda. |
13. |
Ili mkae vizuri migongoni mwao, kisha mkumbuke neema za Mola wenu Mlezi mnapokaa sawa sawa juu yao na mseme: Ametakasika aliye mfanya huyu atutumikie, na tusingeli weza kufanya haya wenyewe. |
14. |
Na hakika sisi tutarudi kwa Mola wetu Mlezi. |
15. |
Na wanamfanyia katika waja wake fungu. Kwa hakika mwanaadamu ni mtovu wa fadhila aliye dhaahiri. |
16. |
Au amejichukulia watoto wanawake katika vile alivyo viumba, na akakuteulieni nyinyi watoto wanaume? |
17. |
Na anapo bashiriwa mmoja wao kwa yale aliyo mpigia mfano Mwenyezi Mungu, uso wake husawijika na hujaa hasira. |
18. |
Ati aliye lelewa katika mapambo, na katika mabishano hawezi kusema kwa bayana…? |
19. |
Na wakawafanya Malaika, ambao ni waja wa Mwingi wa Rehema, ni wanawake! Kwani wameshuhudia kuumbwa kwao? Ushahidi wao utaandikwa na wao watahojiwa! |
20. |
Nao husema: Angeli penda Mwingi wa Rehema tusingeli waabudu sisi. Hawana ujuzi wowote wa hayo! Hawana ila kusema uwongo tu! |
21. |
Kwani tuliwapa Kitabu kabla ya hichi, na ikawa wao wanakishikilia hicho? |
22. |
Bali wanasema: Hakika sisi tuliwakuta baba zetu wanashika dini makhsusi, basi na sisi tunaongoza nyayo zao. |
23. |
Na kadhaalika hatukumtuma mwonyaji kwenye mji wowote ila watu wake walio deka kwa starehe walisema: Hakika sisi tuliwakuta baba zetu wanashika dini makhsusi, na sisi tunafuata nyayo zao. |
24. |
Akasema (Mwonyaji): Hata nikikuleteeni yenye uwongofu bora kuliko mlio wakuta nao baba zenu? Wakasema: Sisi tunayakataa tu hayo mliyo tumwa. |
25. |
Basi tukawalipizia. Angalia ulikuwaje mwisho wa walio kadhibisha! |
26. |
Na pale Ibrahim alipo mwambia baba yake na kaumu yake: Hakika mimi ninajitenga mbali na hayo mnayo yaabudu, |
27. |
Isipo kuwa yule aliye niumba, kwani Yeye ataniongoa. |
28. |
Na akalifanya hili liwe neno lenye kubaki katika vizazi vyake ili warejee. |
29. |
Bali tuliwastarehesha hawa na baba zao mpaka ikawafikia Haki na Mtume aliye bainisha. |
30. |
Na ilipo wafikia Haki wakasema: Huu ni uchawi, na sisi hakika tunaukataa. |
31. |
Na walisema: Kwa nini Qur’ani hii haikuteremshwa kwa mtu mkubwa katika miji miwili hii? |
32. |
Kwani wao ndio wanao gawa rehema za Mola wako Mlezi? Sisi tumewagawanyia baina yao maisha yao katika uhai wa duniani, na tukawanyanyua baadhi yao juu ya wengine kwa daraja nyingi; kwa hivyo baadhi yao wanawafanya wenginewe wawatumikie. Na rehema za Mwenyezi Mungu ni bora kuliko hayo wanayo yakusanya. |
33. |
Na lau isinge kuwa watu watakuwa kundi moja tungeli wajaalia wanao mkufuru Rahmani wana nyumba zao zina dari ya fedha, na ngazi zao pia wanazo pandia, |
34. |
Na milango ya nyumba zao na vitanda wanavyo egemea juu yake, |
35. |
Na mapambo. Lakini hayo si chochote ila ni starehe ya maisha ya dunia tu, na Akhera iliyoko kwa Mola wako Mlezi ni ya wenye kumchamngu. |
36. |
Anaye yafanyia upofu maneno ya Rahmani tunamwekea Shet’ani kuwa ndiye rafiki yake. |
37. |
Na hakika wao wanawazuilia Njia na wenyewe wanadhani kuwa wameongoka. |
38. |
Hata atakapo tujia atasema: Laiti ungeli kuwako baina yangu na wewe kama umbali baina ya mashariki na magharibi. Rafiki mwovu mno wewe! |
39. |
Na kwa kuwa mlidhulumu, haitakufaeni kitu leo kwamba nyinyi mnashirikiana katika adhabu. |
40. |
Je! Unaweza kuwasikilizisha viziwi, au unaweza kuwaongoa vipofu na waliomo katika upotofu ulio wazi? |
41. |
Na hata tukikuondoa, Sisi tutalipiza kisasi chetu kwao. |
42. |
Au tutakuonyesha tulio waahidi. Nasi bila ya shaka tuna uweza juu yao. |
43. |
Basi wewe yashike yaliyo funuliwa kwako. Hakika wewe uko kwenye Njia Iliyo Nyooka. |
44. |
Na hakika haya ni ukumbusho kwako na kwa kaumu yako. Na mtakuja ulizwa. |
45. |
Na waulize Mitume wetu tulio watuma kabla yako: Je! Tulifanya miungu mingine iabudiwe badala ya Rah’mani? |
46. |
46, Na bila ya shaka tulimtuma Musa kwa Ishara zetu ende kwa Firauni na waheshimiwa wake, na akasema: Hakika mimi ni Mtume wa Mola Mlezi wa walimwengu wote! |
47. |
Lakini alipo wajia na Ishara zetu wakaingia kuzicheka. |
48. |
Na hatukuwaonyesha Ishara yoyote ila hiyo ilikuwa kubwa zaidi kuliko nyenginewe. Na tukawakamata kwa adhabu ili warejee. |
49. |
Na wakasema: Ewe mchawi! Tuombee kwa Mola wako Mlezi kwa ile ahadi aliyo kuahidi; hakika sisi tutakuwa wenye kuongoka. |
50. |
Basi tulipo waondolea adhabu hiyo, mara wakaingia kuvunja ahadi. |
51. |
Na Firauni alitangaza kwa watu wake, akisema: Enyi watu wangu! Kwani mimi sinao huu ufalme wa Misri, na hii mito inapita chini yangu? Je! Hamwoni? |
52. |
Au mimi si bora kuliko huyu aliye mnyonge, wala hawezi kusema waziwazi? |
53. |
Basi mbona hakuvikwa vikuku vya dhahabu, au hawakuja Malaika pamoja naye wakamwandama? |
54. |
Basi aliwachezea watu wake, na wakamt’ii. Kwa hakika hao walikuwa watu wapotovu. |
55. |
Walipo tukasirisha tuliwapatiliza tukawazamisha wote! |
56. |
Kisha tukawafanya kuwa watangulizi na mfano kwa wa baadaye. |
57. |
Na alipo pigiwa mfano Mwana wa Mariamu, watu wako waliupiga ukelele. |
58. |
Wakasema: Miungu yetu kwani si bora kuliko huyu? Hawakukupigia mfano huo ila kwa ubishi tu. Bali hao ni watu wagomvi! |
59. |
Hakuwa yeye (Isa) ila ni Mtumwa tuliye mneemesha na tukamfanya ni mfano kwa Wana wa Israili. |
60. |
Na tungeli penda tungeli wafanyia miongoni mwenu Malaika katika ardhi wakifuatana. |
61. |
Na kwa hakika yeye ni alama ya Saa ya Kiyama. Basi usiitilie shaka, na nifuateni. Hii ndiyo Njia Iliyo Nyooka. |
62. |
Wala asikuzuilieni Shet’ani. Hakika yeye ni adui yenu wa dhaahiri. |
63. |
Na alipo kuja Isa na dalili zilizo wazi, alisema: Nimekujieni na hikima, na ili nikuelezeni baadhi ya yale mliyo khitalifiana. Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na mnit’ii mimi. |
64. |
Kwa hakika Mwenyezi Mungu ni Mola wangu Mlezi, na ni Mola wenu Mlezi. Basi Muabuduni Yeye tu. Hii ndiyo Njia Iliyo Nyooka. |
65. |
Lakini makundi kwa makundi yao yalikhitalifiana wao kwa wao. Ole wao walio dhulumu kwa adhabu ya siku chungu. |
66. |
Je! Nini wanangojea ila Saa iwajie kwa ghafla na wala wao hawatambui? |
67. |
Siku hiyo marafiki watakuwa ni maadui, wao kwa wao, isipo kuwa wachamngu. |
68. |
Enyi waja wangu! Hamtakuwa na khofu siku hiyo, wala hamtahuzunika. |
69. |
Ambao waliziamini Ishara zangu na walikuwa Waislamu. |
70. |
Ingieni Peponi, nyinyi na wake zenu; mtafurahishwa humo. |
71. |
Watakuwa wanapitishiwa sahani za dhahabu na vikombe; na vitakuwamo ambavyo nafsi zinavipenda na macho yanavifurahia, na nyinyi mtakaa humo milele. |
72. |
Na hiyo ni Pepo mliyo rithishwa kwa hayo mliyo kuwa mkiyafanya. |
73. |
Mnayo humo matunda mengi mtakayo yala. |
74. |
Kwa hakika wakosefu watakaa katika adhabu ya Jahannamu. |
75. |
Hawatapumzishwa nayo na humo watakata tamaa. |
76. |
Wala Sisi hatukuwadhulumu, bali wao ndio walio kuwa madhaalimu. |
77. |
Nao watapiga kelele waseme: Ewe Malik! Na atufishe Mola wako Mlezi! Naye aseme: Hakika nyinyi mtakaa humo humo! |
78. |
Kwa yakini tulikuleteeni Haki, lakini wengi katika nyinyi mlikuwa mnaichukia Haki. |
79. |
Au waliweza kupitisha amri yao? Bali ni Sisi ndio tunao pitisha. |
80. |
Au wanadhani kwamba hatusikii siri zao na minong’ono yao? Wapi! Na wajumbe wetu wapo karibu nao, wanayaandika. |
81. |
Sema: Ingeli kuwa Rahmani ana mwana, basi mimi ningeli kuwa wa kwanza kumuabudu. |
82. |
Ametakasika Mola Mlezi wa mbingu na ardhi, Mola Mlezi wa A’rshi, na hayo wanayo msifia. |
83. |
Basi waache wapige porojo wakicheza mpaka wakutwe na hiyo siku yao waliyo ahidiwa. |
84. |
Na Yeye ndiye Mungu mbinguni, na ndiye Mungu katika ardhi. Naye ndiye Mwenye hikima, Mwenye ujuzi. |
85. |
Na ametukuka Mwenye ufalme wa mbingu na ardhi na viliomo ndani yake. Na uko kwake ujuzi wa Saa ya Kiyama, na kwake Yeye mtarudishwa. |
86. |
Wala hao mnao waomba badala yake Yeye hawana uweza wa kumwombea mtu, isipo kuwa anaye shuhudia kwa haki, na wao wanajua. |
87. |
Na ukiwauliza ni nani aliye waumba? Bila ya shaka watasema: Mwenyezi Mungu! Basi ni wapi wanako geuziwa? |
88. |
Na usemi wake (Mtume) ni: Ewe Mola wangu Mlezi! Hakika hawa ni watu wasio amini. |
89. |
Basi wasamehe, na uwambie maneno ya salama. Watakuja jua. |