1. |
Ya-Sin (Y.S.). |
2. |
Kwa Haki ya Qur’ani yenye hikima! |
3. |
Hakika wewe ni miongoni mwa walio tumwa, |
4. |
Juu ya Njia Iliyo Nyooka. |
5. |
Uteremsho wa Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu. |
6. |
Ili uwaonye watu ambao baba zao hawakuonywa , basi wao wamekuwa wenye kughafilika. |
7. |
Bila ya shaka kauli imekwisha thibiti juu ya wengi katika wao, kwa hivyo hawaamini. |
8. |
Tumeweka makongwa shingoni mwao, yakawafika videvuni. Kwa hivyo vichwa vyao viko juu tu. |
9. |
Tumeweka kizuizi mbele yao, na kizuizi nyuma yao, na tumewafunika macho yao; kwa hivyo hawaoni. |
10. |
Ni sawa sawa kwao ukiwaonya au usiwaonye, hawataamini. |
11. |
Hakika wewe unamwonya mwenye kufuata ukumbusho, na akamcha Arrahman, Mwingi wa Rehema, kwa ghaibu. Basi mbashirie huyo msamaha na ujira mwema. |
12. |
Hakika Sisi tunawafufua wafu, na tunayaandika wanayo yatanguliza, na wanayo yaacha nyuma. Na kila kitu tumekihifadhi katika daftari asli lenye kubainisha. |
13. |
Na wapigie mfano wa wakaazi wa mji walipo wafikia walio tumwa. |
14. |
Tulipo watumia wawili, wakawakanusha. Basi tukawazidishia nguvu kwa mwingine wa tatu. Wakasema: Hakika sisi tumetumwa kwenu. |
15. |
Wakasema: Nyinyi si chochote ila ni watu kama sisi. Na Mwingi wa Rehema hakuteremsha kitu. Nyinyi mnasema uwongo tu. |
16. |
Wakasema: Mola wetu Mlezi anajua kwamba hakika sisi tumetumwa kwenu. |
17. |
Wala si juu yetu ila kufikisha ujumbe ulio wazi. |
18. |
Wakasema: Sisi tumeagua kuwa nyinyi ni wakorofi. Ikiwa hamtaacha basi kwa yakini tutakupigeni mawe, na mtapata adhabu chungu kutoka kwetu. |
19. |
Wakasema: Ukorofi wenu mnao wenyewe! Je! Ni kwa kuwa mnakumbushwa? Ama nyinyi ni watu walio pindukia mipaka. |
20. |
Na akaja mtu mbio kutokea upande wa mbali wa mjini, akasema: Enyi watu wangu! Wafuateni hawa walio tumwa. |
21. |
Wafuateni ambao hawakutakini ujira, hali ya kuwa wenyewe wameongoka. |
22. |
NA KWA NINI nisimuabudu yule aliye niumba na kwake mtarejeshwa? |
23. |
Je! Niishike miungu mingine badala yake? Arrahmani, Mwingi wa Rehema, akinitakia madhara uombezi wa hao hautanifaa kitu, wala hawataniokoa. |
24. |
Basi hakika mimi hapo nitakuwa katika upotovu ulio dhaahiri. |
25. |
Hakika mimi nimemuamini Mola wenu Mlezi, basi nisikilizeni! |
26. |
Akaambiwa: Ingia Peponi! Akasema: Laiti kuwa watu wangu wangeli jua |
27. |
Jinsi Mola wangu Mlezi alivyo nisamehe, na akanifanya miongoni mwa walio hishimiwa. |
28. |
Na hatukuwateremshia kaumu yake baada yake jeshi kutoka mbinguni, wala si wenye kuteremsha. |
29. |
Hakukuwa ila ukelele mmoja tu; na mara walizimwa! |
30. |
Nawasikitikia waja wangu. Hawajii Mtume ila wao humkejeli. |
31. |
Je! Hawaoni umma ngapi tulizo ziangamiza kabla yao? Hakika hao hawarejei tena kwao. |
32. |
Na hapana mmoja ila wote watakusanywa waletwe mbele yetu. |
33. |
Na Ishara hiyo kwao – ardhi iliyo kufa, nasi tukaifufua, na tukatoa ndani yake nafaka, wakawa wanazila! |
34. |
Na tukafanya ndani yake mabustani ya mitende na mizabibu, na tukatimbua chemchem ndani yake, |
35. |
Ili wale matunda yake, na hayo hayakufanywa na mikono yao! Basi je, hawashukuru? |
36. |
Subhana, Ametakasika, aliye umba dume na jike vyote katika vinavyo mea katika ardhi na katika nafsi zao, na katika wasivyo vijua. |
37. |
Na usiku ni Ishara kwao. Tunauvua humo mchana, mara wao wanakuwa gizani. |
38. |
Na jua linakwenda kwa kiwango chake. Hayo ni makadirio ya Mwenye nguvu, Mwenye kujua. |
39. |
Na mwezi tumeupimia vituo, mpaka unakuwa kama karara kongwe. |
40. |
Haliwi jua kuufikia mwezi, wala usiku kuupita mchana. Na vyote vinaogelea katika njia zao. |
41. |
Na ni Ishara kwao kwamba Sisi tuliwapakia dhuriya zao katika jahazi ilio sheheni. |
42. |
Na tukawaumbia kutoka mfano wake wanavyo vipanda. |
43. |
Na tukitaka tunawazamisha, wala hapana wa kuwasaidia, wala hawaokolewi, |
44. |
Isipo kuwa kwa rehema zitokazo kwetu na starehe kwa muda. |
45. |
Na wanapo ambiwa: Jilindeni na yalioko mbele yenu na yalioko nyuma yenu, ili mpate kurehemewa… |
46. |
Na haiwafikii Ishara yoyote katika Ishara za Mola wao Mlezi ila wao huwa ni wenye kuipuuza. |
47. |
Na wanapo ambiwa: Toeni katika aliyo kupeni Mwenyezi Mungu, walio kufuru huwaambia walio amini: Je! Tuwalishe ambao Mwenyezi Mungu angependa angeli walisha mwenyewe? Nyinyi hammo ila katika upotofu ulio dhaahiri. |
48. |
Na wanasema: Ahadi hii itatokea lini, ikiwa nyinyi ni wakweli? |
49. |
Hawangojei ila ukelele mmoja tu utakao wachukua nao wamo kuzozana. |
50. |
Basi hawataweza kuusia, wala kwa watu wao hawarejei. |
51. |
Na litapulizwa barugumu, mara watatoka makaburini wakikimbilia kwa Mola wao Mlezi. |
52. |
Watasema: Ole wetu! Nani aliye tufufua kwenye malazi yetu? Haya ndiyo aliyo yaahidi Mwingi wa Rehema na wakasema kweli Mitume. |
53. |
Haitakuwa ila ukelele mmoja tu, mara wote watahudhuruishwa mbele yetu. |
54. |
Basi leo nafsi yoyote haitadhulumiwa kitu, wala hamtalipwa ila yale mliyo kuwa mkiyatenda. |
55. |
Hakika watu wa Peponi leo wamo shughulini, wamefurahi. |
56. |
Wao na wake zao wamo katika vivuli wameegemea juu ya viti vya fakhari. |
57. |
Watapata humo kila namna ya matunda na watapata kila watakacho kitaka. |
58. |
“Salama!” Hiyo ndiyo kauli itokayo kwa Mola Mlezi Mwenye kurehemu. |
59. |
Na enyi wakosefu! Jitengeni leo! |
60. |
Je! Sikuagana nanyi, enyi wanaadamu, kuwa msimuabudu Shet’ani? Hakika yeye ni adui dhaahiri kwenu. |
61. |
Na ya kwamba mniabudu Mimi? Hii ndiyo Njia Iliyo Nyooka. |
62. |
Na bila ya shaka yeye amekwisha lipoteza kundi kubwa miongoni mwenu. Je, hamkuwa mkifikiri? |
63. |
Hii basi ndiyo Jahannamu mliyo kuwa mkiahidiwa. |
64. |
Ingieni leo kwa vile mlivyo kuwa mkikufuru. |
65. |
Leo tunaviziba vinywa vyao, na iseme nasi mikono yao, na itoe ushahidi miguu yao kwa waliyo kuwa wakiyachuma. |
66. |
Na tungeli penda tungeli yafutilia mbali macho yao, wakawa wanaiwania njia. Lakini wange ionaje? |
67. |
Na tungeli taka tunge wageuza sura hapo hapo walipo, basi wasinge weza kwenda wala kurudi. |
68. |
Na tunaye mzeesha tunamrudisha nyuma katika umbo. Basi je! hawazingatii? |
69. |
Wala hatukumfundisha (Muhammad) mashairi, wala hayatakikani kwake hayo. Haukuwa huu ila ni ukumbusho na Qur’ani inayo bainisha. |
70. |
Ili imwonye aliye hai, na neno litimie juu ya makafiri. |
71. |
Je! Hawaoni kwamba tumewaumbia kutokana na iliyo fanya mikono yetu wanyama wa mifugo, na wao wakawa wenye kuwamiliki. |
72. |
Na Sisi tukawadhalilishia. Basi baadhi yao wako wanao wapanda, na baadhi yao wanawala. |
73. |
Na wao wanapata kwao manufaa na vinywaji. Basi je, hawashukuru? |
74. |
Na wameishika miungu mingine badala ya Mwenyezi Mungu ili ati wapate kusaidiwa! |
75. |
Hawataweza kuwasaidia. Bali hao ndio watakuwa askari wao watakao hudhurishwa. |
76. |
Basi maneno yao yasikuhuzunishe. Hakika Sisi tunayajua wanayo yaweka siri na wanayo yatangaza. |
77. |
Kwani mwanaadamu haoni ya kwamba Sisi tumemuumba yeye kutokana na tone la manii? Kisha sasa yeye ndio amekuwa ndiye mgomvi wa dhaahiri! |
78. |
Na akatupigia mfano, na akasahau kuumbwa kwake, akasema: Ni nani huyo atakaye ihuisha mifupa nayo imekwisha mung’unyika? |
79. |
Sema: Ataihuisha huyo huyo aliye iumba hapo mara ya mwanzo. Na Yeye ni Mjuzi wa kila kuumba. |
80. |
Aliye kujaalieni kupata moto kutokana na mti wa kijani nanyi mkawa kwa huo mnawasha. |
81. |
Kwani aliye ziumba mbingu na ardhi hawezi kuwaumba mfano wao? Kwani! Naye ndiye Muumbaji Mkuu, Mjuzi. |
82. |
Hakika amri yake anapo taka kitu ni kukiambia tu: Kuwa! Na kikawa. |
83. |
Basi Ametakasika yule ambaye mkononi mwake umo Ufalme wa kila kitu; na kwake Yeye mtarejeshwa. |