1.

Kwa jina la mwenyezi mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu.

2.

Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote;

3.

Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu;

4.

Mwenye Kumiliki Siku ya Malipo.

5.

Wewe tu tunakuabudu, na Wewe tu tunakuomba msaada.

6.

Tuongoe njia iliyo nyooka,

7.

Njia ya ulio waneemesha, siyo ya walio kasirikiwa, wala walio potea.