1. |
Ole wake kila safihi, msengenyaji! |
2. |
Aliye kusanya mali na kuyahisabu. |
3. |
Anadhani ya kuwa mali yake yatambakisha milele! |
4. |
Hasha! Atavurumishwa katika H’ut’ama. |
5. |
Na nani atakujuvya ni nini H’ut’ama? |
6. |
Moto wa Mwenyezi Mungu ulio washwa. |
7. |
Ambao unapanda nyoyoni. |
8. |
Hakika huo utafungiwa nao |
9. |
Kwenye nguzo zilio nyooshwa. |