1. |
Naapa kwa farasi wendao mbio wakipumua, |
2. |
Na wakitoa moto kwa kupiga kwato zao chini, |
3. |
Wakishambulia wakati wa asubuhi, |
4. |
Huku wakitimua vumbi, |
5. |
Na wakijitoma kati ya kundi, |
6. |
Hakika mwanaadamu ni mtovu wa fadhila kwa Mola wake Mlezi! |
7. |
Na hakika yeye mwenyewe bila ya shaka ni shahidi wa hayo! |
8. |
Naye hakika bila ya shaka ana nguvu za kupenda mali! |
9. |
Kwani hajui watakapo fufuliwa waliomo makaburini? |
10. |
Na yakakusanywa yaliomo vifuani? |
11. |
Kuwa hakika Mola wao Mlezi siku hiyo bila ya shaka atakuwa na khabari zao wote! |